Total Pageviews

Thursday, March 27, 2014

Thamani ya mwanamke:Utangulizi

Habari msomaji wangu,karibu katika blogu yangu itayokuelimisha mambo mbalimbali kuhusu mwanamke wa Kiafrika.Lengo na dhumuni ni kuonyesha umuhimu na thamani ya mwanamke katika jamii.
Historia katika jamii ya makabila mengi nchini Tanzania na hata barani Afrika kwa ujumla mwanamke kwa miaka mingi alichukuliwa na kuonekana kama kiumbe dhaifu na kisicho na thamani yoyote ile ile katika jamii.

Hii inatokana na mila na desturi kumfanya mwanamke huyo kama chombo cha kumstarehesha mwanaume,kumzalisha na wengune walienda mbali zaidi kwa kumfanya kama mtumishi wa ndani au kijakazi.

Kama vile haitoshi wanawake hao pia walitumikishwa kama magunia ya kufanya mazoezi kwa vichapo,kashfa,udhalilishaji  unaotokana na mfumo duni na vitendo vingine vichafu ambavyo hapaswi kufanyiwa mwanamke na binadamu yeyote yule.

Lakini kadri siku zinavyokwenda mbele mwanamke thamani yake inasonga mbele katika maeneo mengi ya kisiasa,kiuchumi,utamaduni,mazingira na jamii kwa ujumla.

Wanawake hao kwa sasa hutumia fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii kamavile biashara, kilimo,ufugaji na shughuli nyingine nyingi ambazo wanawake wamekua msaada mkubwa si katika familia zao tu bali pia kwa Taifa kwa ujumla

Wapo wanawake ambao kiutendaji ,taaluma,umahiri na uaminifu wao umekua tegemeo kubwa kwa Taifa letu.Wanawake kwasasa wameshika nyadhifa nyingi serikalini,mashirika ya umma,sekta binafsi hadi ngazi za kimataifa.

Uzoefu u naonyesha mataifa mengi duniani yalio watumia wanawake yamepata ustawi mkubwa sana katika ujenzi wa uchumi wao.Hii inadhihirishwa na uwiano kati ya vijana wa kike na wakiume wanaojiunga katika shule za msingi na za sekondari na hata elimu ya juu.

Wanawake hao  sasa wamethubutu hata kusomesha watoto wao na wengine na wengine kuendesha familia zao.Mbali na msaada mkubwa katika kuendesha familia zao lakini pia msingi mkubwa wa malezi mazuri katika jamii hizo ulitokana na msimamo uliojengwa na wanawake hao.

2 comments:

  1. yeah nazani hii itakuwa ni suluhisho la matatizo mbalimbali yanayomkumba mwanamke hapa tz

    ReplyDelete