Mara nyingi ugumu wa maisha unaonekana kwamtu ambaye amekaa bila kujishughulisha,lakini maisha ni mepesi mno na siku zote naamini mwanamke anayejishugulisha lazima atafanikiwa.
Kukatatamaa ni changamoto ambayo imekuwa ikiwakumba wanawake wengi,matokeo yake wanaishia kulalamikia ugumu wamaisha wakati hakuna wanachokifanya ili kuondokana na hali hiya.
Kuwa jasiri na kutokatatamaa nisilaha tosha kwa mwanamke kufikia maendeleo ambayo wengi wamekuwa wakiyatamani.Uvivu na kutokujiamini ndio sababu inayowafanya wanawake kuendelea kuwa tegemezi na kujiingiza katika biashara haramu.
Siku zote kujiamini na kujipa moyo kwamba nitapambana kwa namna yeyote basi ujue lazima utashinda hatakama hautakuwa tajiri wa kupindukia walau kuweza kujimudu na kuweza kutunza familia.
Mwanamke akiamua anaweza |
Unapojishughulisha kamwe maisha hayawezi kukupiga chenga,hili ni jambo ambalo wamekuwa wakipambana nalo wanawake wengi hasa waumezao wanapofariki dunia,hujikuta wakilia marambili wakifikiria msiba na wakati huo huo wakifikiria ni jinsi gani ataitunza familia
Mwaname ajiwekee misingi ya kuonyesha kuwa anaweza kusimamia na kuendesha familia hata kama mume wake akiaga dunia
Wakati umefika sasa kwa wamawake kuacha kujifungia ndani na kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili kujikomboa kutoka katika wimbi la umasikini.
Ni ngumu kwa mtu anaye kaa ndani halafu atarajie maendeleo,lazima utoke nje kujichanganya na wenzio hapo nidpo utakapokutana na mawazo ya aina tofauti yanayoweza kuwa chanzo cha maendeleo.
Kuna kila sababu ya wasichana kuweza kujiwekea misingi tangu wakiwa wadogo kwa kuzingatia elimu ili kujikwamua katika wimbi la umasikini.
Serikali pia kwa upande wake inapaswa kuwekeza zaidi katika elimu ya watoto wa kike ili kulifanya kundi hilo kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa.
Mwanamke akipewa elimu ya kutosha anaweza kuwa mchango mkubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla,wanawake waliokosa elimu maisha yao yamekuwa yakuhangaika mno.
Kuhusiana na tabia ya wanaume kuwakataza wake zao kujishughulisha hilo ni tatizo kubwa ,mara nyingi hilo linatokana na wanawake kuwa wabinafsi na kushindwa kuonyesha mafanikio wanayoyapata kwa waume zao.
Kuna wanawake licha ya kuwa na mafanikio katika shughuli zao hawataki kushiriki katika maendeleo ya familia,hivyo kujikuata wakikumbana na changamoto kutoka kwa waume zao.
Wapo ambao licha ya kujishughulisha hawataki kuchangia chochote katika familia,ndio maana baadhi ya wanaume hukasirika na kukataza wake zao kufanya biashara kutokana na kutoona mafanikio.
Mwanamke anayetoka anakilasababu ya kuonyesha tofauti na mtu asiye na shughuli,na hilo linatokana na namna ambavyo anajitoa na kushirikiana katika maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.
hakika thamani ya mwanamke inatakiwa kuthaminiwa daima
ReplyDelete