Total Pageviews

Monday, March 31, 2014

MWANAMKE UKIAMUA UNAWEZA

    Mara nyingi ugumu wa maisha unaonekana kwamtu ambaye amekaa bila kujishughulisha,lakini maisha ni mepesi mno na siku zote naamini mwanamke anayejishugulisha lazima atafanikiwa.
    Kukatatamaa ni changamoto ambayo imekuwa ikiwakumba wanawake wengi,matokeo yake wanaishia kulalamikia ugumu wamaisha wakati hakuna wanachokifanya ili kuondokana na hali hiya.
     Kuwa jasiri na kutokatatamaa nisilaha tosha kwa mwanamke kufikia maendeleo ambayo wengi wamekuwa wakiyatamani.Uvivu na kutokujiamini ndio sababu inayowafanya wanawake kuendelea kuwa  tegemezi na kujiingiza katika biashara haramu.
    Siku zote kujiamini na kujipa moyo kwamba nitapambana kwa namna yeyote basi ujue lazima utashinda hatakama hautakuwa tajiri wa kupindukia walau kuweza kujimudu na kuweza kutunza familia.
Mwanamke akiamua anaweza
    Unapojishughulisha kamwe maisha hayawezi kukupiga chenga,hili ni jambo ambalo wamekuwa wakipambana nalo wanawake wengi hasa waumezao wanapofariki dunia,hujikuta wakilia marambili wakifikiria msiba na wakati huo huo wakifikiria ni jinsi gani ataitunza familia
      Mwaname ajiwekee misingi ya kuonyesha kuwa anaweza kusimamia na kuendesha familia hata kama mume wake akiaga dunia
     Wakati umefika sasa kwa wamawake kuacha kujifungia ndani  na kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili kujikomboa kutoka katika wimbi la umasikini.
      Ni ngumu kwa mtu anaye kaa ndani halafu atarajie maendeleo,lazima utoke nje kujichanganya na wenzio hapo nidpo utakapokutana na mawazo ya aina tofauti yanayoweza kuwa chanzo cha maendeleo.

    Kuna kila sababu ya wasichana kuweza kujiwekea misingi tangu wakiwa wadogo kwa kuzingatia elimu ili kujikwamua katika wimbi la umasikini.
    Serikali pia kwa upande wake inapaswa kuwekeza zaidi katika elimu ya watoto wa kike ili kulifanya kundi hilo kuwa na mchango katika maendeleo ya taifa.
    Mwanamke akipewa elimu ya kutosha anaweza kuwa mchango mkubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla,wanawake waliokosa elimu maisha yao yamekuwa yakuhangaika mno.
   Kuhusiana na tabia  ya wanaume kuwakataza wake zao  kujishughulisha  hilo ni tatizo kubwa ,mara nyingi hilo linatokana  na wanawake kuwa wabinafsi na kushindwa kuonyesha mafanikio wanayoyapata kwa waume zao.
   Kuna wanawake licha ya kuwa na mafanikio katika shughuli zao hawataki kushiriki katika maendeleo ya familia,hivyo kujikuata wakikumbana na changamoto kutoka kwa waume zao.
    Wapo ambao licha ya kujishughulisha hawataki kuchangia chochote katika familia,ndio maana baadhi ya wanaume hukasirika na kukataza wake zao kufanya biashara kutokana  na kutoona mafanikio.
    Mwanamke anayetoka anakilasababu ya kuonyesha tofauti na mtu asiye na shughuli,na hilo linatokana na namna ambavyo anajitoa na kushirikiana katika maendeleo ya familia na jamii kwa ujumla.

Thursday, March 27, 2014

Thamani ya mwanamke:Utangulizi

Habari msomaji wangu,karibu katika blogu yangu itayokuelimisha mambo mbalimbali kuhusu mwanamke wa Kiafrika.Lengo na dhumuni ni kuonyesha umuhimu na thamani ya mwanamke katika jamii.
Historia katika jamii ya makabila mengi nchini Tanzania na hata barani Afrika kwa ujumla mwanamke kwa miaka mingi alichukuliwa na kuonekana kama kiumbe dhaifu na kisicho na thamani yoyote ile ile katika jamii.

Hii inatokana na mila na desturi kumfanya mwanamke huyo kama chombo cha kumstarehesha mwanaume,kumzalisha na wengune walienda mbali zaidi kwa kumfanya kama mtumishi wa ndani au kijakazi.

Kama vile haitoshi wanawake hao pia walitumikishwa kama magunia ya kufanya mazoezi kwa vichapo,kashfa,udhalilishaji  unaotokana na mfumo duni na vitendo vingine vichafu ambavyo hapaswi kufanyiwa mwanamke na binadamu yeyote yule.

Lakini kadri siku zinavyokwenda mbele mwanamke thamani yake inasonga mbele katika maeneo mengi ya kisiasa,kiuchumi,utamaduni,mazingira na jamii kwa ujumla.

Wanawake hao kwa sasa hutumia fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii kamavile biashara, kilimo,ufugaji na shughuli nyingine nyingi ambazo wanawake wamekua msaada mkubwa si katika familia zao tu bali pia kwa Taifa kwa ujumla

Wapo wanawake ambao kiutendaji ,taaluma,umahiri na uaminifu wao umekua tegemeo kubwa kwa Taifa letu.Wanawake kwasasa wameshika nyadhifa nyingi serikalini,mashirika ya umma,sekta binafsi hadi ngazi za kimataifa.

Uzoefu u naonyesha mataifa mengi duniani yalio watumia wanawake yamepata ustawi mkubwa sana katika ujenzi wa uchumi wao.Hii inadhihirishwa na uwiano kati ya vijana wa kike na wakiume wanaojiunga katika shule za msingi na za sekondari na hata elimu ya juu.

Wanawake hao  sasa wamethubutu hata kusomesha watoto wao na wengine na wengine kuendesha familia zao.Mbali na msaada mkubwa katika kuendesha familia zao lakini pia msingi mkubwa wa malezi mazuri katika jamii hizo ulitokana na msimamo uliojengwa na wanawake hao.