Ni blog inayokupa nafasi ya kuyatambua maisha halisi ya mwanamke pamoja na malezi ya mtoto, ikiwa ni pamoja na kutambua changamoto mbalimbali katika safari ya kuyafikia malengo yao.
Total Pageviews
Monday, April 14, 2014
MAMA SALMA KIKWETE AKIFUNGUA RASMI MAONYESHO YA WANAWAKE WAJASILIAMALI
Friday, April 11, 2014
MATITI YA WASICHANA 'YAPIGWAPASI KUWAKIMBIZA WANAUME NCHINI KAMEROON

Moja ya mila hiyo potofu ni ile inayoenziwa na jamii nyingi nchini Cameroun na Afrika magharibi
ambayo ipo pia nchini Uingereza na Marekani kwa waafrika kutoka eneo hilo ambao
huyapiga pasi matiti ya wasichana kwa kuyagandamiza kwa mawe ya moto au mchi
lengo likiwa kuondoa mvuto wa wasichana wasifukuziwe na wanaume wakware.
Inasemekana kwa kiasi fulani imepunguza vitendo vya ubakaji watoto ila
kitendo hicho kina athari kubwa kimwili
na kisaikolojia
Mpenzi msomaji wa safu hebu fuatilia
kwa makini kisa hiki kinaonyesha jinsi
gani mtoto wa kike anavyodhalilishwa na kuumbuliwa utu wake
W akati Mick-Sophie
Anne alipoanza kuonesha dalili za kuvunja ungo akiwa na umri wa miaka 10,
mama yake alipagawa kwa hofu ya wanaume kuanza kummendea bintiye huyo mpendwa.
Suluhu aliyoiamini ni kuchukua jiwe lenye moto na
kulishindilia kwa nguvu kwenye matiti ya bintiye katika jaribio la kutaka
kukinyoosha kifua chake ili kuondoa mvuto kwa wanaume.Kila jua lilipotoweka na giza kutawala,aliingia katika jiko lake dogo lisilo na mwanga tayari kwa kumfayia mtoto wake kitendo hicho cha ukatili.
Akiwa humo, Priscille
Dissake anaonekana akiliweka motoni jiwe lenye ukubwa wa ngumi na kisha
kulishindilia kwenye matiti ya bintiye Mick-Sophie
kwa muda wa miezi miwili. Huku dada wa Dissake alionekana akisaidia kumshikilia sakafuni kwa nguvu,ili kuzuia binti huyo asitikisike wakati wakufanyiwa kitendo hicho.
Utafiti mpya wa serikali umeonesha kuwa vitendo vya ‘upigaji
pasi matiti’, kama mila hiyo potofu na haribifu inavyojulikana vimeshuhudia
kupungua kwa vitendo vya ubakaji na ngono kutoka kwa ndugu wa karibu kwa
asilimia 50 tangu vilipofichuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na Shirika la
Ushirikiano wa Kiufundi la Ujerumani (GTZ).
Lakini pia kampeni ya kitaifa ya kujenga mwamko shuleni,
makanisani na katika vyombo vya habari imeweza kuibua uelewa kuhusu athari za
kimwili na kisaikolojia zinazosababishwa na kitendo hicho. Hata hivyo pamoja na kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na wanaharakati, watoto wa kike wapato milioni 1.3 bado ni waathirika wa mila hiyo ya kinyama kwa mwanadamu.
Ni sababu gani hasa ya msingi
inayofanya akina mama hao kuendekeza mila hiyo potofu?
Jibu ni kwamba Kina mama hao wanaendekeza kitendo hicho
kujaribu kuwalinda binti zao dhidi ya ngono za mapema, mimba za utotoni na
ubakaji ulikithiri na kuwauthi akina mama hao juu ya vitendo hivyo
“Mick-Sophie alianza kukua
matiti mapema sana na akawa na mvuto kwa wanaume hususani wakware ambao
wamezoea kutengeneza kuku huku wakiwa na chumvi mkononi
Nilitaka kuulinda
utoto wake na kumlinda dhidi ya wanaume wakware,” alisema Dissake, 46,
akizungumza katika jiko lile lile, ambalo alikuwa akilitumia kuchoma jiwe kwa
ajili ya kuligandamiza katika mwili wa binti yake zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Hata hivyo, juhudi za Dissake za kutaka kumwepusha mwanae
huyo na majaribu hayo hazikuzaa matunda.Katika hali ya kusikitisha na simanzi kubwa kwa maelezo yake mwenyewe na ya mama yake, Mick-sophie alibakwa akiwa na umri wa miaka 13 na mjomba wake.
Mwaka mmoja baadaye alianza kufanya mapenzi na mwanafunzi mwenzake
na akiwa na umri wa miaka 16, alizaa mtoto wake wa kwanza. Mtoto huyo aliyezaliwa wiki sita kabla ya wakati,alifariki dunia saa chache baadaye
Ijapokuwa Cameroon ni nchi pekee, ambayo utafiti wa kina
umefanyika kuhusu upigaji pasi matiti, makundi ya haki za binadamu yanaamini ni
mila iliyoenea sana katika ukanda huo wa Afrika Magharibia.
Aidha wanaamini umeenea miongoni mwa watu kutoka ukanda huo
waishio ng’ambo, ikiwamo katika nchi za magharibi zenye sheria kali za
kuwalinda watoto.
“Sisi Waafrika tunasafiri na utamaduni wetu popote tuendako,
hivyo nina uhakika haya yanatokea Uingereza na Marekani pia,” alisema Margaret
Nyuydzewira, ambaye alizaliwa Bamenda kaskazini magharibi mwa Cameroon, ambako
vitendo vya upigaji pasi matiti ni jambo la kawaida.
Nyuydzewira ameanzisha taasisi ijulikanayo CAWOGIDO, ambayo
inaendesha kampeni dhidi ya upigaji pasi matiti nchini Uingereza, ambako
Wacameroon 9,600 wanaishi kwa mujibu ya sensa ya mwisho mwaka 2011.
Anasema kuna kesi kadhaa za upigaji pasi matiti
zilizoripotiwa katika miji ya Birmingham na London nchini humo kipindi cha
miaka michache iliyopita, lakini idadi inaweza kuwa kubwa zaidi.
“Watu ndani ya jamii zinazoendekeza mila hii wanajua nini
kinachotokea, lakini ukweli unafichwa na kufanyika majumbani.Nikama ukeketaji unajua kinachofanyika lakini kamwe hutamuona yeyote akiufanya".anasema Inatokea nchini Nigeria, Burkina Faso, nchini Chad, nchini CAR (Jamhuri ya Afrika ya Kati) na nchi nyingine za eneo hilo
Hukiita kitendo hiki
kwa jina lingine kwa lugha zao za asili,” anasema. Upigaji pasi matiti ni mila mpya kwa kiasi chake kwani ilianza kupata umaarufu zaidi katika miaka ya 1930 wakati Wacameroon walipoanza kuhama maeneo yao ya vijijini kwenda mijini kusaka ajira, mtaalamu wa tabia na mfanyakazi wa misaada Flavien Ndonko alisema
“Katika majiji haya, kuna kiwango cha chini cha udhibiti wa
kijamii na kimila kutokana na tamaduni tofauti kujichanganya kwa uhuru. Mara wasichana walipoanza kwenda shule na kupata fursa ya kuwa nje ya kaya zao na hivyo pia kupata fursa za kujihusisha na ngono za mapema,” anasema Ndonko, ambaye hufanyaia kazi GIZ.
“Wakati maji safi na mlo bora na huduma za afya zikimaanisha
kukua mapema kwa matiti ya wasichana, na kuwafanya waonekane wakubwa kuliko
walivyo.Wastani wa umri wa ukuaji wa titi kwa wasichana nchini Cameroon umeanguka kutoka miaka 13.5 hadi chini ya miaka 12 kipindi cha miaka 100 iliyopita
Wakati Cameroon likibakia kama taifa la kihafidhina ambako
upataji mimba nje ya ndoa hulaaniwa vikali na utoaji mimba ukiharamishwa, kina
mama hutumia upigaji pasi kama kitendo cha kuhakikisha binti zao hawapati mimba
ana kuacha shule.
Utafiti uliofanyika nchini humo mwaka 2011 umeonesha kuwa
asilimia 20 hadi 30 ya wasichana wa Cameroon huota mimba kabla ya kufikisha
umri wa miaka 16 na thelathini moja huacha masomo yao.Takwimu hizo zinaweza kueleza mwelekeo usio wa kawaida wa kitendo hicho.
Utafiti mpya umeonesha kuwa asilimia 16 ya wasichana hasa
katika eneo la Mbali Kaskazini ambako kuna utamaduni wa ndoa za utotoni
–hujaribu kuyanyoosha matiti yao kwa mawe moto au kwa kutumia mchi ili waweze kuchelewesha
uvunjaji uongo wao na waendelee na shule.
Pamoja na kile Dissake na kina mama wengine wanachosema
kuhusu lengo lao zuri kwa binti zao, bila kujua wanahatarisha kuwaacha binti
zao kwa matatizo makubwa ya kimwili na kisaikolojia, wafanyakazi wa sekta za
afya wanasema.
Utafiti wa serikali uliodhaminiwa na GIZ, ulionesha kuwa
idadi kubwa ya waliohojiwa ilikuwa na matatizo tofauti tofauti ya kiafya
ikiwamo saratani ya matiti.‘Tulibaini kuwa wasichana wenye umri wa miaka 20 waliokutwa na saratani ya matiti,” Ndonko alisema. “Hatujui kama kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya kitendo hicho na saratani, lakini inaibua wasiwasi huo.”
Asilimia 32 ya waliohojiwa walilalamikia maumivu katika
matiti na asilimia 17 walizungumzia kuhusu majipu na vidonda. Asilimia 13 walieleza kuathirika na uzito wa matiti na asilimia nane walipata athari za kudumu za matiti kupinda, kwa mujibu wa utafiti.Athari za kudumu kimwili zinaweza kusababisha athari za muda mrefu za kisaikolojia pia, utafiti ulihitimisha
“Kwa kadiri wasichana wanavyokua na kukomaa, huwa wawezi
kuonesha matiti yao kwa marafiki wa kiume na au waume zao,” Ndonko alisema.
‘baadhi ya wasichana hujihisi aibu kufanya ngono bila kuondoa nguo zao kutokana
na kuficha matiti yao yenye kasoro.”
Lakini wote Ndonko na Nyuydzewira wanaamini kina mama
hawapaswi kuchukuliwa hatua bali waelimishwe athari za kitendo hicho.“Tunapaswa kuwaelimisha kwanza na kuwaadhibu pale tu watakapoendelea na kitendo hicho,” alisema Nyuydzewira.“Tunapaswa kuwaelimisha kwanza na kuwaadhibu pale tu watakapoendelea na kitendo hicho,” alisema Nyuydzewira.
Kuwaadhibu kina mama kunaweza kuwa kitu kigumu kwa sababu
wasichana wengi wanaamini mama zao wako sahihi kwani wanawalinda.‘Inafaa kuanza na kina mama kwa sababu binti zao bado ni wadogo wanakubali kwa hofu au sababu ya heshima kwa wazazi wao,” alisema
Kuhusiana Dissake baada ya kuelimishwa alijihisi kuwa na
hatia na kukiri kwamba alifanya kosa bila kujua akidhani anafanya kitendo cha
busara.“Upigaji pasi matiti unaumiza sana kuliko uzaaji,” anasema Mick-Sophie Anne. Nimsamehe mama yangu, lakini kamwe sitasahau hili,” anasema.
Subscribe to:
Posts (Atom)